Listen to Mwanamalundi by Fid Q

Mwanamalundi

Fid Q

Hip-Hop/Rap

1,056 Shazams

Lyrics

Mwanamalundi! Ah Niite ngosha the don, niite mwanza mwanza Love me. or leave me alone Nakipakaza unaposema hukomi, nami Simwoni wa kujitandaza juu, ya kitanda hiki cha mziki We hujui utanishangaza, wanakoshwa! Masikioni wanaposikia hizi ladha Inawachosha inavyo'hit redioni nyomi inajaza Mashabiki, zaidi ya milioni hadi wakusaza dah TMK, Ilala na 'Ndoni wanamjua mwanza Ambaye ame'base na hiphop kama saigon wa zavaragwanza Naenda mlipa kama scratch zina bony love jibaba homie Na'keep on top, Mcee slash hustler Kwenye hip naweka hop kisha naiteka ki'mafia Chapchap. nonstop hits je we utabaki. Jinsi nnavyozi'drop machizi, chicks wanafagia Tamu kama lollipop, rhymes nnazoshusha Situmii kalamu, kichwani hapohapo natungia Natumia ufahamu wa hii fani, maisha kuyashuhudia Naangalia angani naona amani inaniambia dereva ntabeba msalaba begani usukani nikiuachia Niite Ngosha the don, au Mwanza Mwanza au Mwanamalundi Mwanamalundi Mwanamalundi Mwanamalundi Kuna makeups, pia mkorogo Kuna haters, na wale waliojiskia tu kuleta shobo Kuna tofauti kati ya Mcee na CEO, Tambi na minyoo Glass na kioo Bafu na choo SKIA, ili usisahau ONA, ili ujifunze FANYA ili ukumbuke kama ulisahau ya jana Wafurahishe walio karibu, walio mbali watasogea Elewa, kama mbwa, usijaribu hata kuongea Unachokitaka haukipati, aliyekipata hakitumii Hapo ndipo utapodata na mashauzi ya plan b Mikakati ya kiusanii na wakati wa bahati nasibu Sio lazima kipaji ili mradi mshakaji anahitaji kitu Atasukumaje siku? Huyu mzugaji mzinguaji siwezi kumpa Huyu wakati Mungu ndo mpaji, unakosea hii Wanatumia mbaya za bandia kurudia viporo Ushapagawa, watoto sasa wanasaka chochoro Hapa kahawa, ni maji ya moto yenye rangi ya ugoro Hatuwezi kuwa sawa, mwendo wa kasoro zenye kasoro Uhuru wa miguu mikono, akili imefungwa mnyororo Ntawadhuru sana huo usingizi wa pono tommorrow Hauna ushuru mdomo, chunga ulimi usilete mgogoro Ona, bila farasi kidume hawezi kuitwa Polo Niite Ngosha the don, au Mwanza Mwanza au Mwanamalundi Mwanamalundi Mwanamalundi Mwanamalundi
Writer(s): Fareed Kubanda Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out