Lyrics

Mhhh, mhhhh Mi kwako sikuingia miguu Mikono hadi kichwa kiufupi mazima Nikiamini wa kufa kuzikana Yani hoi isio nafuu Maututi kabisa hata mashaka siiina Nikiaminiiii tutatengwa na Maulana Mvumilivu hula mbivu Nimengoja mpaka zikaoza Naambulia maumivu Ingali sina wa kupoza Sijui yangu stahamilivu kumnyenyekea kwaniponza Napambania utulivu mwenzangu chuki unaikoza Sikukufuta tu machozi ulipolia nililia na wewe Sa mbona wanilipa majonzi Yani stress mapombe nilewe We ndo wangu Yesu Mkombozi Sa mbona Petro unaniacha mwenyewe Nikose usingizi na njozi ndo ufurahi Ok sawa si unataka nitukanwe Ongeza, ongeza badooo (Nidhalilike) Ongeza, ongeza badooo (Nikose pa kuificha sura) Ongeza, ongeza badooo (marafiki wanicheke) (Waning'ong'e hadaa) Ongeza, ongeza badooo Mmmhh kisichokuua hukukomaza eti kiuskali huo msemo mi nakataa Mana jua linapoangaza ndo sina afadhali mie kwangu ni mabalaa Oooohh najitahidi kumsinga mwali ila somo ananikataa Ooohhh penzi letu si la kibatari anayamwaga mafuta ya taa Kutwa ni vurugu ndani Purukushani hapakaliki Roho inaniuma yani kwa nini sa tunagombana sweet Ooohh jema gani nambie labda nitende kipi Hata pa kucheka honey eti utani unapaniki Naelewa ridhiki mafungu saba na la kwangu sita Naelewa sikutoshi labda kukuridhisha Sikukufuta tu machozi ulipolia nililia na wewe Sa mbona wanilipa majonzi yani stress mapombe nilewe We ndo wangu Yesu Mkombozi Sa mbona Petro unaniacha mwenyewe Nikose usingizi na njozi ndo ufurahi Ok sawa si unataka nitukanwe Ongeza (eheeeee), ongeza badooo (eheeeeee) (Nidhalilike) Ongeza, ongeza badooo(eee) (Nikose pa kuificha sura) Ongeza, ongeza badooo (Ndugu jamaa wanicheke, waning'ong'e hadaa!) Ongeza, ongeza badooo (ehee) Nikose pa kuificha sura Ah, waning'ong'e hadaa...
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out