Lyrics

Ooii naona mkandaa unakatika Uko kimya sana mkato au kundi limevunjika Na utanyooka raundi hii Na hivi huwezi bila mimi? Najikuta JAY Z oya unarudi lini? Kaka, huku wamefunga mipaka Ila tiketi nilikata nirudi kabla pasaka Rudi ugeuze kisu sio Mwana kulitafuta mwana kulipata Raundi hii sio ununio Daraja la,,,, Basi kumekucha Ni saa ngapi huko nipe takwimu Nimeamka nishaweka bundle Namwongoja Ummi Mwalimu Anapambana yule dada Tanga nimewavulia kofia Wametoa sanitizer za iliki Yaani ukipata unalipia Corona nishai Yaani bongo kila mtu daktari Maasai kachemsha majani Ya mpapai kanywa na sukari Buza hadi maski wanafua Sijui nani kawafundisha Huku kuna dada kajifukiza Mashetani akayapandisha Tueke siasa kando Unajuwa uchumi unashuka? Sio bongo tu hadi ng'ambo Watu wamefunga maduka Hapa nawaza pesa ya pango Benki waliokopa wanajuta Tukisema tukae ndani Na hii njaa si tutakufa? Hali inatisha na umaskini Tunaoumia ni sisi Yaani bora ufe kwa ukimwi Angalau utaandika urithi Kwa hiyo hamna bata Sio kidimbwi sio tipsi Kaka madanga wamekata So hazitimbi hizo pisi Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega Nani kama wewe? Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega Nani kama wewe? Hivi unakaa jimbo gani Au Marekani ya vijijini Unajikinga vipi maana Vifo vingi hadi siamini Mmm au umesharudi Uko zako rohoro nini? We bana ebu niache Mi nimeze Chloroquine Umenikumbusha Kwani Chloroquine ni dawa? Bado inafanyiwa uchunguzi Ila haijathibitishwa Ingawa ukinywa Haitatarisha Ndio maana bado wanaigawa Mi nakunywa maana Nilishika uso kabla ya kunawa Eti unaweza kawa nayo Na usionyeshe dalili? Ewaa, uko sahihi Na kingine kuhusu hili Ni kwamba mgonjwa wa corona Unaweza usimtambue kwa macho So mtu yeyote unamwona mpe mita mbili toka kwako Na hiko kifanslika Ndio kinini baba Willy? Ni Ventilator ni machine Ka mapafu ya nje ya mwili Sijaelewa, embu nieleweshe Kuhusu hili, nasikia vinauzwa ghali Basi vile vingi mwimbili Okay, kirusi cha corona Kinashambulia mapafu Ndipo zinaanza homa, mafua ya kifua Halafu unashindwa kupumua Na mwili unahitaji dafu Ventilator huingiza hewa Na kuitoa iliyo chafu Tuepuke mikusanyiko Ikibidi tukae ndani Tumeambiwa tujifukize Hivi ni dawa unadhani? Ngoja kwanza Hivi fumigation Mmm mmm Baba ile inaua mende Acha utani Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega Nani kama wewe? Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega Nani kama wewe? Maisha ya upweke yanasumbuwa Ila siku zinapita Yule mkewe itunze pete mtayamaliza Na uhakika kaka Ila hatua dua Haina haja ya kusikitika Ila navyokujua Kweli hujazini miezi sita Kiukweli mi mwaminifu Ingawa jogoo anawika Mama Ivanny mabalifu Hakuchiti una uhakika? Kuna mchezaji wa yanga Namuona anapita pita Nitamkata kata mapanga Yaani namuua na namzika Oyah wape nyumbani Basi pesa ya matumizi Kaka nitoe wapi Na show hakuna sikuhizi Hali imekuwa ngumu Hakuna pesa kila corner Kila mtu unayemdai Naye anasingizia Corona Mbona sasa wanafunga shule na vyuo Halafu bar hawafungi Mzazi atamlindaje mtoto Na akirudi na akirudi yupo tungi Polisi India wanapiga watu wakisongamana Wao wabarakoa wanajua hadi fender wamebanana Sasa wanatukusanya kutuambia tusikusanyike Ila wauguzi wanajitoa sana Duh, Mungu awalipe Wapinzani mnatangaza vifo Walopona hamwatangazi Wanasema mungeeka takwimu Za wazi ingekuwa kizazi Kwa hiyo lockdown hakuna Halafu umeona texti niliotuma? Ipi? kwenye group Mbona inbox hakuna? Nasikia, nini? Kwa Yuzee Kambochi Maana huko uliko usiongee Sana inatosha Hadi papai lina Corona! duh Kaka Tuchati Mmm na mbuzi vipi? Ee eh Kaka Tuchati Mwili umekufaa ganzi Kaka Tuchati Poa mwanangu tundelee kujifukiza
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out