Lyrics

Tumekumisi Roma Rudi Nyumbani Uwatetee Wanyonge ndugu zako Uwakumbushe Sasa sijui nianzie wapi kifuani nimebeba mengi Na sitotenda haki nisiposema hiki sipendi Hiki napenda kile sitaki mambo ya kishenzi Tanzania haijaezekwa bati na wamekula pesa ya ujenzi Yaani nchi wanaifanya mti mjenzi anauona mbao Ndege ataona makazi mkulima ataona mazao Mganga atauona dawa na mpishi atauona kuni Ataemiliki mwenye power sisi atatusagia kunguni Na ukisema hawatufai wanakuumiza uwe mpole Yaani wanaangua papai kwa kutumia gobole Mnatumia nguvu kubwa kwenye mambo madogo Jeshi gani mpaka leo mmeshindwa kumjua kigogo Tukiongelea kutekwa eti tunarudia ajenda Hamjibu mnakwepa mbona mama anarudia kilemba Nchi gani raia akihoji mnasema anakosoa Na akikosoa anatukana serikali hii sio poa Haya basi tuseme mko sawa na mna nia nzuri na sisi Mbona vyuma vimekaza halafu mama anaificha grease Mara mkapandisha tozo kampeni mkono hatuwaungi Si tulihoji mkajibu kwa dharau tuhamie Burundi Tatizo mkishaapishwa tu mnawaza uchaguzi ujao Hamuwazi njia mbadala ya kumlinda mkulima na mazao Sasa Iringa si tuna maitu halafu tuspick twaagiza china Manaake hapo kwanza ncheke yaani bongo kikubwa uzima Sa mnatuambia tujiajiri mbona nyinyi hamkujiajiri Okay nikupe boda yangu kisha we unipe uwaziri Nikukabidhi vyeti vyangu hangaika navyo mwezi mmoja Niko pale nakujgoja uje tuongee lugha moja Mi sio CCM sio Chadema hili niliweke wazi Ila ukiweka CCM na Andazi ntachagua Andazi Simuamini mtawala na mpinzani simsadiki Maana wanaendelea kukatika huku deejay kauzima Mziki Na inaniuma kuona msomi wa degree tatu Nashindwa kumpa ajira sasa anauza nyanya karatu Sasa sijui mtaniua nikimshikia mama shilingi Maana hata inyeshe mvua mnasema anaupiga mwingi Na ninamkubali na nitamng'ata sikio kama hujui Wanaomkosoa ndo wanampenda wanaomsifia ndo maadui Ili wapate teuzi ndo wanamlamba miguu Wakimpamba hawamsaidii Amiri Jeshi Mkuu Tunakupenda Roma Tunakumiss Roma Rudi Nyumbani Roma Utusemee Tunakupenda Baba Tunakumiss Mwana Tunakukumbuka sana Hivi hamjasikia tetesi kuwa remote iko msoga Si huku mageng imedoda magogoni imenona Watu tatu ndani ya track moja wamekalia kigoda Ngolo Kante anampa Mbape cross anafunga Pogba Hii nchi ina wenye nchi walanchi na wananchi Na kuendelea kuwachagua ni kwenda na mchanga mbichi Tuwajaribu wapinzani watawala si wameshapata Ugoro umewaingia puani sasa ona wanapiga chafya Wanatumia dollar kubaki kuongoza dola Watawafunga watapora wataua watahonga vijora Karatasi tunaibiwa za kura kwenye sanduku Kwa hiyo mnatuonyesha ziwa huku mmeziziba chuchu Okay kura ziko 300 na kuna watu mia kwa jimbo Na kituoni hakukua na watu halafu wameshinda kwa kishindo Sa kama Askofu mfufua watu ameiba kura za wapinzani Je atashindwa kuiba sadaka za kura kanisani Hii ni gani mchungaji akitaka gari twamchangia Muumini akitaka gari anaombewa tunamsalia Sa mchungaji tusimpe pesa tumuombeevna yeye pia Tukae pale tusubiri miujiza ya wagalatia Wabunge wengi mlishinda kwa hisani ya mwendazake Mkipatacho muende Chato mkumbuke hata ndugu zake Jimbo hili haliendelei cause mmemchagua mpinzani Haya sasa mmeshinda kote fauluni huo mtihani Turuhusu siasa za amani turudi zile enzi zetu Uchaguzi sio siku moja ni mchakato wa muda mrefu Mikutano ya nje na ndani ndo tunaimarisha chama Daily mtulishe majani halafu sikukuu mtupe shawarma Keki ya taifa ni kubwa tuache siasa za risasi Mnawaonea wakishika dola watalipa kisasi Tulipotoka ni mbali siasa za mwendazake Msirudi msilale chali huku mnatutemea mate Na BASATA msikie hili msije fungia huu wimbo Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo Sawa tulinde maaduli ila tusiue wabunifu Mtupende tunaokosoa kama mpendavyo wanaosifu Wengine wamekuwa viongozi na mliwaona tu marapper Hiphop ni mkombozi na sauti isiyo na mipaka Ushauliza kwanini bega lipo karibu na kwapa Usiondoke baki hapa usikie verse inayofuata Tunakupenda Roma Tunakumiss Roma Rudi Nyumbani Roma Utusemee Tunakupenda Baba Tunakumiss Mwana Tunakukumbuka sana Nawashangaa vijana warembo na watanashati na nusu Wanaosema bila mlengo eti siasa haiwahusu Mwanasiasa anaweza amua tu na ukalala mahabusu Mnakosea wadogo zangu na kamwe sitoruhusu Siasa ndo inaamua sukari iuzwe shingapi Na inapanga kaliua ni wapi wajenge zahanati Na ijue tofauti ya mwanasiasa na mwanaharakati Mmoja ndo mzalendo mwingine maslahi binafsi Ntawafundisha kitu kabla hajawika jogoo alfajiri Pesa unayonunua maduta mkate unaolipa bili Hoja yake inamlipa Raisi Polisi Mbunge Waziri So una haki ya kuwakosoa maana we ndo umewaaajiri Tatizo hatuna ujasiri na akili tumekaza fuvu Vipi nitafuzu kichwa suzuki engine ya Isuzu Anayechelewesha msafara siku zote ni ng'ombe wa mbele Ila anachapwa wa nyuma na ndo anayepiga kelele Na mjenga katiba mpya sio BAWACHA wala BAVICHA Eti wabonngo maji sio katiba mnawaficha Haya sasa hayo maji yako wapi mbona hamuongei Uko wapi umeme mmebugia kiazi cha mtoto Mdomo unacheza sebene Katiba iliyopo ni bora ipa ni bora kwa watawala Ukipinga wanakupa keai na hauna hela kibatala Kwa mwamvulu wa maendeleo wanahairisha mchakato Mbona mkoloni alijenga miundombinu yote hapo Na ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne tu Uongozi bora, siasa sadi, Ardhi na watu Yanga na Simba ni wapinzani ila sio kwamba hawapatani Maji yanayotoka mto msimbazi ndo yanayojaza jangwani Na hiyo ndo amani tuitakayo sisi sio vurugu Tunataka kuona Januari anamgongea fegi sugu Hakika naacha glasi ya Bapa mezani anaenda msalani Anamuachia mwigulu anarudi na anakunywa kwa amani Na sio utani msipojifunza hapa ndo basi tena Aliyesema aomgezewe muda bungeni ndo ameaga mapema Wakamlisha asali kwa kisu akalamba akamwaga wino Tangulia na dereva barua utaikuta chamwino Mi nitakufa mimi ila ngoma zangu zitaishi Na mtakuja na mashada siku yangu ya mazishi Nipeni maua yangu niyanuse angali nipo hai Nikiondoka mnikumbuke msilie bali mfurahi Tunakupenda Roma Tunakumiss Roma Rudi Nyumbani Roma Utusemee Tunakupenda Baba Tunakumiss Mwana Tunakukumbuka sana
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out