Lyrics

Maamuzi yako nimatokeo ya kesho Amua vema upate mema wewe Maamuzi yako nimatokeo ya kesho Amua vema upate mema wewe Alikuwepo mama mmoja ngoja niseme Jina lake aliitwa Tundo Alisumbuliwa na ugumba miaka mingi Ndoa yake ilikuwa matatani Hata mawifi zake wote hawakumpenda tena Tundo aliamua kwenda kwa waganga Alizunguka huku na kule kutafuta msaada Aliona bora aende kwa waganga Tundo Maamuzi yako matokeo ya kesho Amua vema upate mema wewe Alikutana na mganga mmoja nchini Congo Akampa dawa za kutosha Tundo Tundo alizaa mtoto wa kiume Jina lake alimwita Sinduna Maajabu aliyokuwa nayo mtoto yule Alikuwa amezaliwa na meno Maajabu aliyokuwa nayo Sinduna Alizaliwa na meno kama mtu mzima Tundo kwa kuchelewa kwake alifurahi Akaamini mganga amemsaidia Lakini alipokuwa akinyonyesha mtoto yule Ghafla alimng'ata mwili wake Tundo Mwili ukapoa wote upande mmoja Lilikuwa ni tatizo lililomsumbua Tundo Maamuzi yako matokeo ya kesho Amua vema upate mema wewe Tundo alilia akisema mwili wangu wote sasa umebadilika Rangi ya ngozi yake Tundo Iligeuka ikawa gamba la nyoka mwili mzima Siku moja marafiki zake Wakamtembelea Tundo Siku moja ndugu zake walipomtembelea Tundo Wakalia sana Wakamwambia ndugu yetu Tundo Tuna muhubiri anahubiri twende ukaombewe Tundo Maamuzi yako matokeo ya kesho Amua vema upate mema mama Maamuzi yako unayochukua Amua vema upate mema Tundo akaondoka na mtoto wake Huku tatizo la utasa limekwisha Akifurahia kumuona mtoto Alipokuwa muhubiri akihubiri Alimuona Tundo mbele yake Akamwambia mama njoo mbele Tundo akasogea akijua muujiza umefika Akamwambia Tundo njoo mbele Tundo akijua Mungu amesikia Mchungaji akauliza Muhubiri akauliza Umebeba nini mgongoni mwako Tundo? Kwa ujasiri Tundo akasimama akasema Nimebeba mtoto wangu anaitwa Sinduna Kwa ujasiri Tundo akasimama Akasema nimebeba mtoto jina Sinduna Muhubiri akamwambia Tundo Mshushe mtoto wako hapa kwenye madhabahu Akaomba kwa imani sana Mtoto aliageuka chatu mara ile Eti Sinduna sio mtoto Kumbe Sinduna ni chatu Kumbe Sinduna sio mtoto Kumbe Sinduna ni nyoka kubwa Maamuzi yako nimatokeo ya kesho Amua vema upate mema wewe Muhubiri akamwambia Tundo Mchukue mtoto wako sasa Watu wote kwenye mkutano wakakimbia Wahandishi wa habari wakapiga picha Ni kweli unaweza kushangaa Lakini ndiyo yaliyomkuta Tundo Wahubiri waliposimama wakamwabia Nenda kamwite mume wako Mume alipokuja akaambiwa Huyo ndiye mtoto wako Sinduna Yule baba alilia sana Akasema mganga mganga Ule baba alilia kwa uchungu Akasema kumbe Sinduna Yule baba alilia sana Akasema mungu wangu eh Akalia kwa uchungu akilaumu Kumbe mganga ametudanganya Kumbe Sinduna sio mtoto Kumbe sinona ni nyoka kubwa Kumbe Sinduna sio mtoto Kumbe Sinduna ni nyoka kubwa Lipo jibu lipo Maishani mwetu lipo jibu Yesu jibu yupo Maishani mwetu yupo Katika magumu tuna yo pitiya Yesu ndilo jibu Katika aza tunazopitia Yesu ndilo jibu Muujiza upo upo Maishani mwangu upo Macho yangu yameona Muujiza wangu unakuja Macho ya rohoni yameona Baraka zangu zinakuja Moyo wangu mimi unanisudia Baraka zangu zipo zina Acha Baraka za kipepo zipite Ziko baraka toka kwa mungu zinakuja Lipo jibu lipo Maishani mwako lipo jibu Lipo jibu lipo Hata kama limechelewa lipo Jibu la maisha yako lipo Jibu jibu eh Jibu la tatizo lako Jibu lako bado lipo Lipo jibu lipo Maishani mwetu lipo jibu Yesu jibu Yupo Maishani mwetu yupo jibu Lipo jibu lipo Maishani mwetu lipo jibu Yesu jibu Yupo Maishani mwetu yupo jibu
Writer(s): Bahati Bukuku Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out