Lyrics

Kweli mizani ya hadaa ni chukizo baya Ni uangamivu ulio karibu, Mtu mjinga huamini kila aambiwalo bali mwenye hekima hufikiri sana, Apendaye mafundisho hupenda maarifa bali achukiaye ni kama mnyama, Mtu mjinga huamini kila aambiwalo Kijapo kiburi huja aibu, Yuko wapi rafiki yako mlopendana siku ya kwanza mlipokutana, yuko wapi? Aliyesema anakupenda mpaka kifo kiwatenge leo yuko wapi rafiki yako? Alikupa ahadi nyingi na viapo tele, leo yuko wapi rafiki yako? Mbona amekukimbia umebaki pekee yako unahuzunika pole we! Alisema anachanganyikiwa, nisipoiona sura yako leo yuko wapi rafiki yako? Alikuja na vicheko na furaha tele, leo yuko wapi rafiki yako? Mbona unateketea ah, unaangamia amekwenda zake rafiki yako! Tumemwona mtaa wa pili Anakwenda zake amekusaliti rafiki yako! Wenye dhambi wakikushawishi mwanangu kataa usiwafuate utaangamia, Watakuja na maneno mazuri tamu kama asali usiwasikize ni walaghai, Watakuja wenye sura zuri tena mvuto wa ajabu usiwatazame ni walaghai, Hata wawe na shape nzuri, zuri kama nini, usiwatazame utaangamia! Kucheza na marafiki wabaya epuka mwanangu ni sawa na kushika sikio la simba! Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo 'tavunjika ghafla hapati dawa MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Rafiki yako, MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Anakulaghai MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Rafiki tapeli MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Rafiki wabaya MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Rafiki yako, MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Japo anacheka nawe, MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Japo anatembea nawe, MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO _Anawinda roho yako, MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU! _Rafiki mwema, NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU _Pendo lake la milele, NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU _Yeye huponya magonjwa, NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU _Jina lake ni faraja NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU _Wamwendeao wanapona NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU _Ukimwita anaitika, NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU _Ukimwita anaitika, NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU _Sikio lake si zito, NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
Writer(s): Rose Muhando Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out