Lyrics

Mungu kwetu ni kimbilio wakati wa shida Msaada uonekanao wakati mateso Mungu kwetu ni kimbilio wakati wa shida Msaada uonekanao wakati mateso SOLO1 Wapendwa na tuamini kwamba Mungu wetu tupo Tena anayajua majira na nyakati hizi Wapendwa na tuamini kwamba Mungu wetu tupo Tena anayajua majira na nyakati hizi SOLO2 Hakuna jambo linalotokea kwa bahati tu Bali kila majira kuna kusudi la Mungu (Majira haya Mungu baba) Mungu umeisimamisha dunia kwa nguvu zako Umezinyamazisha ndimi zetu umefunga midomo yetu Na mbio za miguu yetu (Taratibu za maisha) Zimebadilika hata taratibu za kukuabudu wewe Mungu zimebadilika pia SOLO 3 Wewe hulali wala husinzii Unaujua mwanzo wetu hata mwisho wetu Wewe hulali wala husinzii Unaujua mwanzo wetu hata mwisho wetu SOLO 4 Kimbilio letu tumaini li kwako eeh Mungu Maana ufahamu wetu na akili Vimefika mwisho. Nguvu na mamlaka za dunia haziwezi kamwe Sayansi maarifa haviwezi kushindana nawee yahweh Tuvushe tuvuke katika mapito Kama ulivyowavusha wana Israeli katika bahari ya shamu Tuvushe tuvuke katika mapito Kama ulivyowavusha wana Israeli katika bahari ya shamu SOLO 5 Bado lipo tumaini kwa kila aaminie Lipo tumaini Bado lipo tumaini kwa kila aaminie Lipo tumaini (Kwa Yesu) Kwako lipo tumaini, kwako (Kwako Bwana hatubanduki) Kwako lipo tumaini, kwako (Matatibu wanatibu lakini) Kwako (Yesu) lipo tumaini, kwako (Uponyaye ni wewe Bwana) Kwako lipo tumaini, kwako (Dunia yote mikononi mwako)
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out