Lyrics

Shukrani ya punda-JAHAZI MODERN TAARAB Oooh aaah Oooh Wahenga wameona mbali sana, Ya kuwa punda shukrani hana Na haya yamenipata, Leo Mimi nayaona Kiumbe mbebe uwezavyo, Katu hatotulizana Kweli binadamu, Tumekosa uungwana Instrumental... VERS: 1 Oooh aaah Tenda wema uende zako shukrani usingoje Si lazima wema wako ulotenda uuongoje Tenda wema nenda zako shukrani usingoje Si lazima wema wako ulotenda uuongoje Jua mja hana shukrani, hili linajulikana Hata umtendee nini, Pia shukrani hana Bora fuga mbwa ndani, Mwaweza saidiana Kuliko ya hiisani, Mtakuja kugombana Bora fuga mbwa ndani, mwaweza saidiana Kuliko ya hiisani, Mtakuja kugombana Wako waja wana shukrani ya punda Wako waja wana shukrani ya punda Shukrani ya punda mateke, ya punda mateke Ndo wafanyavyo, wafanyavyo Mwenye uungwana wake, uungwana wake Hafanyi hivyo, hafanyi hivyo Hukumbuka wahisani wake, wahisani wake Ndivyo ilivyo, ndivyo ilivyo Instrumental... VERS: 2 Aaah ooooh Oooh aaah Kwa nililowafanyia kwa imani, mmeyaapa kisogo Safi yangu nia, toka moyoni Mmeyafunga virago×2 Shukrani zenu, hazina mkia Wa kuwaoongoza, muendako Niliyoyafanya, kwa kujitutumua Yote mmeyatupa huko Bado mwanisilibia, Na kuongeza vituko Mola atanilipia, Madhali sipo mlipo Bado mwanisilibia, na kuongeza vituko Mola atanilipia, madhali sipo mlipo Duniani tends wema usisubiri malipo×2 Shukrani ya punda mateke, ya punda mateke Ndo wafanyavyo, wafanyavyo Mwenye uungwana wake, uungwana wake Hafanyi hivyo, hafanyi hivyo Hukumbuka wahisani wake, wahisani wake Ndivyo ilivyo, ndivyo ilivyo Instrumental VERS: 3 Ooooh aaah Aaah oooh Sana inauma ufanye wema, shukrani usipewe Tena inachoma yote mema, laawamani utiwe×2 Katu sikati tamaa, kutenda mema kwa waja Mola ndiye anayejua, matendo ya kila mja Mimi kimya nnakaa, sitopenda kujifuja Nataka kuendelea, na wema wangu kwa waja Mimi kimya nnakaa, sitopenda kujifuja Nataka kuendelea, na wema wangu kwa waja Shukrani ya punda kweli mateke×2 Shukrani ya punda mateke, ya punda mateke Ndo wafanyavyo, wafanyavyo Mwenye uungwana wake, uungwana wake Hafanyi hivyo, hafanyi hivyo Hukumbuka wahisani wake, wahisani wake Ndivyo ilivyo, ndivyo ilivyo Intro Tenda wema kwangu nia, shukrani usitendewe Ubaya utaambulia, wema wako ufungiwe Roho haitataharuki, kutenda wema kwenu nyie Wema hakupata nyuki, iweje nipate mie Tenda wema kwangu nia, shukrani usitendewe Ubaya utaambulia, wema wako ufungiwe Mshipa haunitoki kukosa shukrani zenu Kwangu mambo la msingi, siyafati yaloyenu Tenda wema kwangu nia, shukrani usitendewe Ubaya utaambulia, wema wako ufungiwe...
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out