Lyrics

Nimetafakari habari zako nami nashindwa kuelewa kabisa Binadamu angenipa neema kesho angechoka kunipa zaidi Lakini wewe hauna kikomo, wala mvua yako haina majira Bwana, wanyesha mvua, Bwana, kwa walio jangwani Bwana, wawasha jua, Bwana, mpaka baharini Kweli Bwana wewe ni mwema sana nitasimulia miji, Yesu ni mwema, Yesu ni mwema Nitahubiri vijini, Yesu ni mwema Yesu ni mwema Nitayafafanua haya, Yesu ni mwema Yesu ni mwema Watu wote wapate kuyajua, Yesu ni mwema Yesu ni mwema Nitasimulia nchi, Yesu ni mwema Yesu ni mwema Niliwaza kwa ubinadamu mpaka mwisho wa kufikiri Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu Kwa kuwa humtupi anayekutumainia Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe Uzoefu wa mapito haya ukaninyima usingizi Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu Kanuni za dunia zikavunja matumaini Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe Giza lilipotanda mchana likanifunika usoni Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu Nikapiga kelele hofu kuu ikanisonga Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe [T|b] Naimba he he, naimba leo Naimba he he, naimba mimi Ulijua wazi kwamba mimi sikuwa nastahili, Kwa sababu mimi mdhaifu mwili na roho Ukaruhusu nifanikiwe juhudi zangu Makusudi ili nione ukuu wako Ndugu wanipende, jamaa waniheshimu Marafiki wanijali, wanisaidie Ndiyo maana leo, mimi nakurudishia; [W] Utukufu ni wako milele Sifa heshima ni vyako daima Wewe peke yako unastahili Usifiwe na uhimidiwe! Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante Nakupa utukufu, kwa kuwa umeniona asante Milele na milele, kwa kuwa umeniona asante Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out