Lyrics

Keeping the good music alive Thats my job! I like the way y'all lookin' tonight Wow! This is the.eer.kind of music you can twist up to I mean like.er.to the left, to the right Step it up, to the right, C'mon! Left, right Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani (kama kama kama kama zamani) Natamani iwe Eeh! (Lets Go!) Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani (kama kama kama kama zamani) Natamani iwe Eeh! (Feel me!) Sikukukosea nilikukosea kuamua Nkadhani umenikosea sana nkashindwa kuchagua Machozi yangu na maumivu yana uhusiano unajua Nawezafanya chochote rudi maa Mungu anajua Bado sinywi pombe kama ulivyoniacha shuga Huwa naswali ila sifungi mawazo yamenipa ulcers Wananicheka ujinga 'coz nakuongelea wewe tu Nikiongelea mapenzi mfano wangu wakwanza ni wewe boo Kama ni ndoto naomba Mungu iishe mapema Naona mateso ka' naibeba dunia nzima Nashindwa kula nashindwa kulala mama Kila kukicha naumia kama tuliachana jana Ni jeuri tu zinaniumiza Yasingefika huku kidume nisingeendekeza Mara ngapi nilikosea mimi na ukanisamehe Mara ngapi ungeweza kuliacha penzi lipotee Hukuniacha ukaganda na mimi kama ulinizaa wewe Nilishindwaje kusamehe wakati ulipokosea nawe! Tungeachana usiku tukarudiana asubuhi Jeuri tu zinaniongoza nashindwa hata kumsabahi "Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani (kama kama kama kama zamani)— MwanaFa Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani (kama kama kama kama zamani) Natamani iwe Eeh! (Lets Go!) Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani (kama kama kama kama zamani) Natamani iwe Eeh! Siwaulizi shosti zako kama bado unanikumbuka Siwezi majibu yao ya shombo yatanisuta na ntawachapa Sijasahau walivyonibembeleza enzi tunavunjika Na nilivyogoma kuwasikiliza wote vicheche nkawaita Sikuwa na uwezo wa kuku-treat kama millionaire Mapenzi yakazidiwa na maisha we had to break somewhere Yes ulinikosea na ukanifanya nkalia Nkashindwa kujikaza ikanibidi kukuachia Hukuamini maneno yangu hukupenda the way they sounded Au labda ahadi zangu hazikufikia what you wanted Kama nkupigie simu nkusikie tu itanitosha Hata ukinitukana moyo wangu utaupumzisha (baby come back) Kama wakati urudi nyuma uniombe msamaha tena Ama usingenikosea tuishi kama zama Ukirudi sikuachi uende tena Hata ukinikosea ukafanya ka' uliyoyafanya tena Nani atafanya nisikuwaze? Hakuna binti wa aina yako Nsasamehe ulikosea tu rudi kwa nafasi yako (rudi maa!) Sileti tena kisu kwenye mpambano wa bunduki Shell silingi tena taka sitaki sasa basi Nikikaa chini waza mengi juu yako Na some times, na-miss sana hot kisses zako Natamani niguse tena mwili wako Penzi lako, natamaniiiihh kama zamaniiii!! Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani (kama kama kama kama zamani) Natamani iwe Eeh! Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani (kama kama kama kama zamani) Natamani iwe Eeh! One more time. Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani Natamani iwe Eeh! (Lete kwaya sasa!) Oh oh oh! natamani iwe, natamani iwe kama zamani Natamani iwe... Eeh!
Lyrics powered by www.musixmatch.com
Get up to 2 months free of Apple Music
instagramSharePathic_arrow_out