Lyrics

Je, umekumbuka kumuombea Yule umpendaye? Jamani twazingirwa na maovu mengi Kwa hiyo inatupasa, kuombeana sana Mtoto wako, atoka asubuhi sana Kwenda shule, sokoni na kadhalika Apitapo kumejaa mabaya mengi sana Mama, mwombee mtoto wako Mwombee mtoto wako Apitapo ajali ni mingi Mbwa wakali wamzingira Siku hizi vibaka ni wengi Oh, mwombee mtoto wako Ewe mama, watenganishwa Na mume wako kaenda safari ya mbali kikakazi Je, umemwombea Kule aliko mbali nawe? We kumbuka amezingirwa na maovu mengi Mwombee mume wako Kule nasikia kuna wachawi Na wenzake kumwonea wivu Keelewana na mabosi zake Afya njema asiugue Ewe Baba watenganishwa Na mke wako kaenda safari ya mbali shuleni Je, umemwombea kule aliko mbali nawe We kumbuka amezingirwa na maovu mengi Mwombee mke wako Kamwombee sana mke wako Aweze kufaulu shuleni Majaribu mengi yampata Uvumilivu kwa kila jambo Oh, mwombee mtoto wako Oh, mwombee mume wako Oh, mwombee mke wako
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out