Lyrics

Yea, yea, yea, yeah Baba nitafutie kazi huko serikali Ka kuna ka nafasi niwekwe pahali Aki ya nani sitaambia mtu huku Baba shida yangu tu ni ya mapato Si unishikanishe na ka Parastatal Wakiniita tutaonana kando Vijana wanataka kazi Wana elimu, nguvu na vipaji Lakini Kenya hii si kumejaa wajuaji Kupata kazi huku ni roketi sayansi Vijana wanataka kazi Kwani maisha ngumu bila kazi Sasa Nairobi mji umejaa majambazi Ni wengi wanategemewa nyumbani Wafanye aje? Mama nieleze wapi naweza ni ka apply Je kuna kandarasi tunaezawai? Nikuulize, si unajuanga mtu huku? Mama, mambo yako nitakuona hii weekend Mi sina noma na kugawa Per diem Weh wakumbushe tu ni postiwe huku Vijana wanataka kazi Wana elimu, nguvu na vipaji Lakini Kenya hii si kumejaa wajuaji Kupata kazi huku ni roketi sayansi Vijana wanataka kazi Kwani maisha ngumu bila kazi Sasa Nairobi mji umejaa majambazi Ni wengi wanategemewa nyumbani Wafanye aje? Na sikupenda kwetu ni vile hali Inaleta pressure ni kitu gani hii Sikupenda kwetu ni vile hali Inaleta pressure ni kitu gani Kupata kazi imekua kazi Wasichana wanataka mtu anakazi Watoto wanataka NAN, wipes na diapers Maisha kweli ni ngumu bila kazi
Lyrics powered by www.musixmatch.com
Get up to 2 months free of Apple Music
instagramSharePathic_arrow_out