Lyrics

Mitaa inapangusa usingizi wa macho yao Makorongo wananyoosha mabawa yao Wasukumaji mikokote wanapakia vigari vyao Bodaboda wanapangusa mavumbi pikipikini Mitaa inapangusa usingizi wa macho yao Makorongo wananyoosha mabawa yao Wasukumaji mikokote wanapakia vigari vyao Bodaboda wanapangusa mavumbi pikipikini Tena, jua linakucha Kampala Asubuhi inaanza tena Licha ya kila kitu, licha ya kila kitu Tena, jua linakucha Kampala Asubuhi inaanza tena Licha ya kila kitu, licha ya kila kitu Watu, si mbali na hapa, huamka na njaa bado Watu, si mbali na hapa, huamka na njaa bado Matatu wanachanja njia, kama kawaida Wakristo wanahubiri kuhusu haki takatifu Matajiri wanameza tone la bia yao baridi Jua linawaka migongoni mwa wafanyakazi Tena, jua juu ya vichwa Kampala Adhuhuri imefika tena Licha ya kila kitu, licha ya kila kitu Tena, jua juu ya vichwa Kampala Adhuhuri imefika tena Licha ya kila kitu, licha ya kila kitu Watu, si mbali na hapa, hufanya kazi na njaa bado Watu, si mbali na hapa, hufanya kazi na njaa bado Solo# Eno ye Kampala yaffe Okwabwobwe eeh Tulinga momboze Akasente kambirigo Akokulya okukafuna Ndulu Omwaana womuntu Nga alabye Waadhini wanawaita kwenye swala ya Isha Umeme umeenda, giza linakuja mitaani Mama wanawaita watoto nyumbani Maduka ya mwisho yanafungwa Tena jua linakuchwa Kampala Siku moja inamalizika tena Licha ya kila kitu, licha ya kila kitu Watu, si mbali na hapa, hulala na njaa bado Watu, si mbali na hapa, hulala na njaa bado Tena jua linakuchwa Kampala Siku moja inamalizika tena Licha ya kila kitu, licha ya kila kitu Licha ya kila kitu, licha ya kila kitu
Writer(s): Oğuz Tarihmen Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out