Lyrics

(1.) Sikuyajua kama ndivyo yalivyo, Mpaka roho aliponionyesha, Shetani navyo jua kujigeuza, Kama malaika yule wa nuru, Meji-geuza mekua rangi nyingi, Meji-ingiza kwa siri kanisani, Watu wa Mungu wao bila kujua, Ata wameanza kumuabudu. Waraka wa Yohana ule wa kwanza, Sura ya tatu mstari wa nane, Azitendaye dhambi ni wa shetani yeye, alizitenda tokea mwanzo. Tunao watu wengi makanisani, Kutenda dhambi kwao sio tishio, WAKIKUTANA PAMOJA KUABUDU, SWALI MNIJIBU WANAMWABUDU NANI? (2.) Kutoa pesa kwao sio tatizo, Hawajaolewa waendelea kuzaa, Hawajatubu dhambi wanazitenda, Tena ni viongozi wa kina mama, Hata kanisa wao ndo walojenga, Wanadhani ni mikutano ya nje, WAKIKUTANA PAMOJA KUABUDU, SWALI MNIJIBU WANAMWABUDU NANI? Fungu la kumi kutoa sio shida, Lakini wameoa mabibi wengi, Mchungaji kitaka kosana nao, Awaambie watubu dhambi. Gari la kanisa wao ndo linunua, Na pia vyombo kupasia sauti, WAKIKUTANA PAMOJA KUABUDU SWALI MNIJIBU WANAMWABUDU NANI? (3.) Na wahubiri nao sio kidogo, Ni washirika kumbe ni wake zao, Wamewakuta watu wamesimama, Wanawaangusha wawaibie. Wanahubiri ujumbe wa kutoa, Wanasahau toba ya msamaha, WAKIKUTANA PAMOJA KUABUDU, SWALI MNIJIBU WANAMWABUDU NANI? Na makanisa mengine ya ajabu, Wokovu wa Yesu wanaukataa, Ule wa pombe kwao sio waajabu, Ata mchungaji anaibariki. Ukiwambia wewe umeokoka, Wasema hiyo sio imani yao, WAKIKUTANA PAMOJA KUABUDU, SWALI MNIJIBU WANAMWABUDU NANI? (4.) Giza na nuru zina shirika gani? Toeni giza katikati ya nuru, Tumuabudu Mungu Mtakatifu, Katika Roho na pia Kweli. Yesu ni Kweli tena ndiye Uzima, Na njia ya kutufikisha mbinguni, Mungu ataka zote tumuabudu, Katika Roho na pia Kweli. Ewe shetani pepo uliye mchafu, Nakuamuru kwa jina lake Yesu, Toka ndani ya kanisa lake Mungu, Uende kuzimu kachomwe moto, Tumegundua ila na njama zako, Tukuabudu wewe ni kama nani? Tunaye Mungu Baba yetu Yehova, Sifa utukufu ni wake milele.
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out