Lyrics

Imekuwa muda sasa papa sijakuimbia Lingala Baba Nimekuwa nikishughulisha na mareggea na maragga Mablues zikafanya mimi n'kalala Sasa nimeamka Baba naimba Lingala Waliniambia lingala poa nifunge mshipi juu ya tumbo Na nijue kilingala eti "petit Lingala le eza moke" Wakaniambia Lingala poa niongee katikati ya wimbo "Naongea, na sina kitu cha kusema" Mimi nasema Lingala ya Yesu haikuwangi complicated Ukipewa kagitaa tu Unainua mikono juu, unasifu Yesu juu Lingala ya Yesu wangu, inaokoa Lingala ya Yesu wangu, inabariki Lingala ya Yesu wangu, si complicated Unasifu Yesu juu Sio lazima utoboe kila pahali ndio msanii usikike Sio lazima magari ya kifahari ndio video ishike Sio lazima ujue kilingala ndio Congo ufike Nao madancer, nguo zimewabana, zimewabana Mimi nasema Lingala ya Yesu haikuwangi complicated Ukipewa kagitaa tu Unainua mikono juu, unasifu Yesu juu Unasifu Unasifu Unasifu juu Sio jina lako we msanii, unasifu Yesu Juu
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out