Lyrics

Imani nafsi inaniambia Haukuwa fungu langu Na sidhani kama nilikosea Kuukabidhi moyo wangu Ulinidanganya mapenzi ni zuri basi Panda twende safari Bila kujua la kwako ni mwendo kasi Ghafla ukanipa ajali Upweke umetawala nafsi Mwenzako usiku silali Ninahesabu mabati Kisa wewe Sijutii moyo wangu Kupenda nisipopendwa Sirudii makosa yangu Ujinga wakati wakwenda Kinachoniuma roho yangu ooh Kuwapa neno wahenga Maana si kwa posti zangu Na kujinadi napendwa Nishapona, nishapona Nishapona ila mazoea Basi nenda umwambie Nishapona! Oooh mwambie Basi umwambie eeh Nishapona ila mazoea Heshima kunyenyekea Nilivyomnyenyekea Akaniona si chochote kwake Mazima akanipotezea Akanipotezea, alipomaliza shida zake Na bado siamini kweli ndo yule Alokuwa akisema, halali asiponiona Na kujilisha ya nini? Yote ni bure Nikamwita chanda chema, alinidanganya Zile miziki za kunichombeza, zinaniuma roho Mara akinidekeza, elaji njoo Ungesema nilipoteleza, nikamwomba koo Si vyema amenitelekeza mb kisadooo Basi nenda umwambie, nishapona! Oooh mwambie Basi umwambie eeh Nishapona ila mazoea Basi nenda umwambie, Nishapona! Oooh mwambie Basi umwambie eeh Nishapona ila mazoea Nenda kamwambie naja Nenda kamwambie naja Basi nenda kamwambie naja Nenda kamwambie naja
Writer(s): Rajab Kahali Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out