Lyrics

Hodi wenyewe Nacha ndo nagonga Namuulizia ndoa hivi nimemkuta au katoka Ala kumbe yupo mwite namhitaji huku Naitaka sana ndoa ila tatizo najishuku Nataka kujua pia nimekuja kukuuliza Na kama ndoa ni tamu ni kwanini inawaliza? Ni kwanini inawaumiza bado najiuliza Na ni kwanini baada ya ndoa majuto hupitiliza Wanandoa wengi hawana furaha Na wengi wao mara nyingi tunakutana sana bar Nakata tamaa jirani kila siku zogo Na na mbona wanandoa wengi wana nyumba ndogo? Kipi ni sababu ya wanandoa kugombana? Kitandani hana kipya kwaiyo hana tena maana? Aliamua kukuigizia na kuwa kakupenda sana Au mlikurupuka kipindi cha uchumba nyinyi mkaoana Inanipa wasi inaniwia vigumu Kuamini nikioa ndoa yangu inaweza dumu Mawazo yananikumba nikiwaza kuingia ndoa Nachohofia ni kuingia ule mlango wa kutoka Hata maji ya moto kuna muda yanapoa Hakuna kitu kibaya kama kukosea kuoa Sorry kwa usumbufu ila nilitaka tu nipime Nitarudi tena wacha nigonge hodi kwingine I'm coming home Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo Coming home, waambie Milango yote inanikataa Acha nijaribu siasa majitaka taka Dini kabisa hofu napata pata Ndoa kabisa imenikataa Ngoja nigonge mlango wa dini nitatue haya mafumnbo Nijue kinagaubaga sitaki kufuata mkumbo Mi sio Isaka, Yakobpo wala Musa mwenye fimbo Wanafanya kwa faida ya Mungu au faida ya matumbo? Nijitie mkosi na nijisahau Na mwisho nikapige goti chini mbele ya madhabahu Au nijivike ugaidi ukaidi hayawani Au niwe na busara kama mfalme Suleimani Mlango nyeti hadi kuingia tu naogopa Mnanishauri niji Macca au mchungaji wa kuokoka Nikiingia huku kuna vitu nitavikosa Starehe za kidunia unadhani wapi nitapata? Mmenipata? Na nacho ogopa Ni kumjaribu Mungu kwa kuingia na kutoka Nimkane kama Petro nimsaliti kama Yudah Niutangaze ufalme wa Mungu mbele yao nikiwa shuhuda Niingie kupata pesa 'NO' moto utanichoma Au niingie kuitangaza injili kila kona Toa ndugu toa, toa ulichonacho Ninunue Prado mpya nongeze kipato Ogopa kuwa Mungu wakati we mwenyewe una Mungu Siku Mungu akikasirika dunia utaiona chungu Kuabudiwa kama Mungu na unajua we sio Mungu Ni kutafuta mchawi nani na unajua mchawi ndugu I'm coming home Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo Coming home, waambie Milango yote inanikataa Acha nijaribu siasa majitaka taka Dini kabisa hofu napata pata Ndoa kabisa imenikataa Kila mlango ni mgumu sioni pakukimbilia Najiuliza kwanin ni lazima ndani mi kuingia Kabla sija ghairi nakuna kichwa faster Nawaza nikagonge labda mlango wa siasa Naskia ni mchezo mchafu sitaiweza mi ni msafi Naogopa kulaghai watu mwisho wakipati Naogopa tega ndoano niwavue hawa samaki Na mwisho nishibe mimi niwanyime wao haki Au niingie huenda naeza kuwa bora ka Nyerere Bora ka Mandela nifikishe nchi mbele Nikifa nikazikwe kwa shujaa Butiama Au kaburi langu likazikwe Nyasubi Kahama Kabla sijaingia kuna vingi niliona Kura za haki bao la mkono Maradona Kwa Mungu sasa nitachosema nini? Ikiwa nilikula nikasaza nikasahau walio chini Siasa ina makali kama kisu Nikikumbuka alivyotakaga kuuawa Nafikiria kutekana nafikiria kuchafuana Na ndicho naogopa sana I'm coming home Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo Coming home, waambie Milango yote inanikataa Acha nijaribu siasa majitaka taka Dini kabisa hofu napata pata Ndoa kabisa imenikataa
Lyrics powered by www.musixmatch.com
Get up to 2 months free of Apple Music
instagramSharePathic_arrow_out