Lyrics

Leo nalivua pendo nililopenda zamani Nabadilli wangu mwendo nami niwe furahani Nimechoshwa na skendo, vita na purukushani Kweli asiyejua pendo apendwapo hapaoni Nilimpa kwa kishindo penzi lote la moyoni Raha na wingi uhondo sikumnyima mwandani Ameyavunja kwa nyundo mwenzenu sikuamini Leo nalivua pendo nirudi yangu thamani X2 Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo Hatuwezi kulingana kauli hata matendo Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo Niliyajenga kwa nondo mapenzi yangu ya ndani Kwa ufundi na miundo na mambo yote ya Pwani Kumbe nalea uvundo aibu tupu nyumbani Kweli asiyejua pendo hapendeki ni shetani Pendo gani la magendo apendwae hafanani Leo naliweka kando pendo hili la kihuni Najiepusha na lindo kumlinda hayawani Kwani mapenzi mkondo hayataki ushindani yeah X2 Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo Hatuwezi kulingana kauli hata matendo Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo Nimehitimu msondo, msondo wa kizamani Nikahusiwa upendo, upendo siri yake nini Nimefundwa kimitindo, na starehe za chumbani Kupendana ni matendo, mtendeane hisiani Kweli mchezea jando, mapenzi kwake ni nini? Bora niyapige tindo, mimi nawe buriani X2 Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo Hatuwezi kulingana kauli hata matendo Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
Lyrics powered by www.musixmatch.com
Get up to 2 months free of Apple Music
instagramSharePathic_arrow_out