Lyrics

Rudi nyumbani kapumzike Rudi nyumbani kapumzike Nimeshindwa na maudhi Rudi nyumbani kapumzike Ukishabadilika utarudi Maana haya mahusiano yananipoteza Haya mahusiano yananipoteza Najua we' ni mrembo na machoni unapendeza Ila una haraka na kwenda na kasi yako sitaweza Umeanza kuigeza jinai Eti nipate nguvu unanilisha pweza na chai Haujui habari ulizosoma zimewekwa masilahi Umeshika simu sana mpaka umenipoteza walahi Ukiona mashati mabuti unapagawa Na miili ya movie ambayo wame-boost na madawa Unataka niache kazi na mimi nishinde gym niji-boost Eti niwe kama Jux unanigawa Umepumbazwa hutaki shika kisomo Unakubali kila kitu hujui mengine ni promo Nilikuwa nakuridhisha leo unataka nikuridhishe Mara mbili kwa kunifananisha na wacheza ngono Unaniambia sinukii fresh inanilazimu Ninunue marashi ya gharama toka Zenji Toka enzi, nahisi mpenzi una wazimu Unanidharau sababu ya maisha unayo-check kwenye simu Haki ya mama ukweli, uwongo sibongi Tangu umepata hiyo simu msosi boko sikosi Usiku mzima una-chat kelele ndoto sioti Eti unajiita princess Jojo kidoti Kwanini usiache drama tuishi ka' zamani? Hizi kashikashi zinanichanganya Mara unilambe mara utake ku-kiss hadharani Kisa kina flani walifanya Ushanitia nuksi tangu tanga zama Tungeweka kifusi cha mchanga ukachagua harusi ya kisasa Ukalia machozi nikavunga nikakusikiliza Mpaka sasa tunaishi kwenye nyumba ya kupanga Kisa unasema dunia tunapita mpango gani huu Ndani hatuna hata akiba ya pesa ni vidani tu Sitasahau siku madeni ya harusi bado sijalipa Ukalazimisha nikope ili twende honeymoon Honeymoon Huu upendo unaniliza ah! Huu mwendo umenishinda Nimepaka rangi upepo nimekupenda wewe Wakati unapenda urembo kupitiliza Nimegundua hii hujuma sitanyamaza Mpaka sipeleki tena huduma tena kwa maza Baada ya miaka kadhaa ya kwenye nimegundua Huu upendo wangu unanilemaza Zikwapi enzi zako Kazi umefukuzwa maana masihara yameshusha weredi wako Njaa ikija tuuze hereni na cheki zako Au tuuze samani ili kulipa madeni yako Kutumia pesa za akiba ndio wazimu kabisa Kodi ikija haitalipwa na hizo timu za Twitter Mke wangu umejua jiji, mpaka najiuliza We ni nani? Kwa maana mke wangu hakua hivi Nimeshachoka ona sura yangu inajieleza Wakati nakuoa tabia yako ilipendeza Namtaka mke wangu wa mwanzo yule niliyempenda Sio huyu anayemsalimia maza kwa kiingereza Vile unaniona mpole unajivika mapembe Nilikupa uhuru sasa unanishika makende Hii tabia uliyoianzisha inanisikitisha na nimeshindwa Sa' nazila nisepe Angalia rafiki zangu, kisha linganisha na rafiki zako Hasa ambao wanaomzunguka binti yangu Huwa nawaza wanachomfundisha ni nini? Zaidi ya umbea kunywa pombe na kupiga vimini Mama hao rafiki zako washaoza Hakuna afadhali hata mmoja Wanapenda sana maisha ghali nilikupa taadhali ukae mbali Hukukubali, yule mrefu alishawahi kunitongoza Anajua nimekuoa nimefunga mageti yangu Nisingemkubali hata angenikuta enzi zangu Ananishika kila akinikuta peke yangu Anasema umemwambia kuhusu ukubwa wa nyeti zangu Asa' ndo' nini? Sijui Kuruthumu sijui Martha Mrefu mweusi yule mwenye tatoo kwenye paja Ni mpumbavu sana anajikuta anajua Ana mdomo mchafu sijui ka' anaulia chakula Mbele ya mtoto anatukana ka' pepo Anajua viungo vyote maana alishalala hadi central Kila mtoto wetu huwa napata mateso Unataka tulee mtoto au malaya wa kesho Wema hauna gharama mahususi Ila pindi unapotenda ubaya Jua ubaya utarudi hauwezi kuitabili kesho hata uwe special Dunia duara mama acha kujifanya mjuzi Siku ambayo yatakuhama makundi Na mimi nitaumwa sana niko ndani nimelazwa mahututi Na pesa hamna ya kununua kiganja cha chumvi Jirani hawezi kuja maana ushamtukana matusi Walishasema wanazuoni "ashakum si matusi" Si matusi mke wangu, walishasema Nyuma ya mwanaume masikini kuna Mwanamke mpumbavu Pesa tulizopoteza sio kinachoniuma Pesa zipo na zinatafutwa Sio gari, sio nyumba kinachoniuma Umenipotezea time na siwezi kuurudisha muda Umeiweka kweli sababu ya maisha ya ndoto Umekumbatia uongo unaishi kama mtoto na Umekua umefungua milango ya kejeli Elimu ya jando na unyago zimefeli Rudi nyumbani kapumzike Rudi nyumbani kapumzike Rudi nyumbani kapumzike Ukishabadilika utarudi
Writer(s): Edger Vicent Mwaipeta Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out