Lyrics

Oya Mwela alikuja nikampiga sound mbumba mbaya Siwezi lala down town naitunza kaya Niko around ninavunja taya Michongo kibao town wana hawakuvuta waya Achia jala Ni heri kuyashinda majaribu Ila kufeli ni kushindwa kujaribu Baba alifeli siwezi feli pia Namiliki jina la ukoo sio sheli dia Siwezi lala njaa itanigaraza Kwahiyo usiniletee risala achia jala kwanza Sina kazi nimedandia ndala Alafu unanikazia fala Bro achia Jala Hauna shida ndo' maana unapendeza Alafu unaniambia hauna fedha Sikupi kichaka sikupi hata stata utakimbia Achia jala ntakupiga mitama utajifia Sikupenda kuwa vikundi vya wahuni Nilikuwa madini ambayo hauyakuti vitabuni Nilikuwa mtu kabla enzi zangu Haya maisha yangu ni kitabu na hii ni peji chafu So achia jala Dingi mwenyewe alitoboka Madeni kama dhambi milele nakokota Na alipodondoka nikarithi shida Ndio maana Kuelewa mtu lazima uelewe alipotoka Achia jala Sichezi kamali na washua Nitakupiga kabali nitakuua, sikuachii hata ukisali Matumaini yako mbali Nami nipo katikati ya bahari na mashua Hauwezi kuwa mtoto ukishazaa Nina mtoto sasa, sitaki kuuza ndoto ka bidhaa Mwanzo nilikuwa na ndoto na iling'aa Lakini bahati mbaya mtoto hawezi kula ndoto ikija njaa Nilipenda kuwa rubani Ila mambo ni makubwa ukubwani Nikaishia kuwa mkulima fani niliyofunzwa nyumbani Kabla shamba halijakumbwa tufani So achia jala Nimekufata tangu Benki najua kuwa una cash Uliingia ukiwa empty ukatoka na mabegi Una-act kama ndezi Unaniletea undezi nitakuletea ushenzi wewe Nilichora plan na sikupiga mchele Wenzangu wa mtaani ni'shawazika tele Najua unahesabu time ujaribu kurun sijui Nimeshika gun nitakuchezea shere Achia jala Siwezi kudanganya kuhusu Haya Madusko hatuwezi kugawana nusu Usihubiri sisadiki maadili Maisha yenyewe mafupi na hatuishi mara mbili Achia jala Mbunge halijui jina langu Ramani ya jiji haisanifu njia zangu Hawajivunii ndugu zangu, Miungu haisikii sauti yangu Niko peke yangu mimi na gun yangu Nitaku pah pah Kisha unione mamluki Nitakuchezesha mabuzuki Nishafungwa mara tatu nimetoa roho nne Utakuwa wa tano, so jaribu kutoka nduki nikuonyeshe Nipo kazini so achia jala Nitakutia ngwara ufe Mafanikio ni kwa wale majasiri Walio tayari kusubiri ni makupe Nisikize brother Ni'shafanya mamziki Sikuvutia kukusanya mashabiki Naogopa kuwa begi nishazika marafiki Nilishalala na maiti nishajiuza kwa shangingi Nishafunga mahirizi, nishakula mamizizi Nishafuga Jinamizi mamisuba nikasizi Nishakuzwa na waizi waliokuzwa na machizi waso Mama ananiona failure for life Na ninamisi kumbatio la wife Mkwe ananiona bwege, napeleka nuksi malangoni pake Shemeji ananiona sio type So achia jala, nitakubia roho nipe jala Usinizoee usinipe gwara Unahisi sina maadili ninafata mkumbo bwege Huwezi kuwa consious ukiwa tumbo empty Achia jala Sijarithi mali ili nizichunge kama zako Jala ziko mbali nizifuge Kama zako Wajomba masadali sio wabunge kama wako Sijaenda shule yako I'll fucking shoot you, Achia jala Nimeshindwa leo sio kwamba nilisinzia jana Sijakwambia kwamba alisinzia baba Hakujua mkwanja ni maua mazuri yanafifia ghafla Achia jala Hey, so sad hunijui boy, am not your Calibre Usituone tu tajiri, wengi tuna suck blood ki-Cannibal Msimamo kitaliban, na roho ya kijahidina Kama mbwai mbwai ndio utajua mi kikosi kama Pina But I won't choose that hata ka' niko street smart Nna-pure fact nahisi we ni mgonjwa unahitaji meds Mental disturbed maybe afya ya akili Na uko so bitter it's not healthy unapoteza asili Hata mi nili-hustle man same thing na Bakhresa Niliogopa pressure sikutafuta demu ilikua pesa Hata nikitesa,don't judge me that's my money Nyie waishiwa pesa mnatoaga advice kwani? Plus I got my family ambayo inanitegemea Na nasimama kama nguzo kwa nyumba wakiegemea Hata hapa umenisimamisha tu kuna muda unapotea Najua unapitia mitihani, ila kikubwa nitakuombea Bidii ni mazoezi tenda kwa muda uone matokeo Mafanikio yatakuja hakuna aliyezaliwa akiwa na cheo Ukipata wekeza ndio sababu sikupenda vileo Na kupunguza maninja ndio ueze kumkumbatia mkeo Nikutolee form mimi twende huku Kuna form Maisha kutafuta nilipo nilisepa home Blacks you don't have to bend knee ki uncle Tom Upo kwa era wanaompenda ndio hawajui ku perfom Kuhusu muziki labda huku-appeal kwa soko poa Au whatever product ulitoa zilikuwa zinaboa Ulihitajika kuwa na strategy na market iliyobora Sio upate mchongo tu kisa ni Kenwari bora wa kuchora Na usi blame wazazi kikubwa ni kukuleta uhaini Unavyokua jambazi wana blame kwanini walizini Na kukupata wewe ambae una act mwewe hufugiki Halafu skia kwanza haunitishi nishaishi hata na mungiki Na kuua sio fani something u boss for Unajilaani damu mikononi and we both know Jiulize hizi roho ziliko zinamwambiaje mungu Na ubani unachomwa Familia zikikumbuka machungu Dogo sitakujenga leo twende tukajenge We the first civilization mbona tufe kisenge Ukiacha jembe Sahau kuhusu sembe Usinichanganye boy tukadhani mamba,kumbe kenge Na kama wataka kuniua basi fanya fasta Ila kumbuka nitakaowaacha hawatakuacha Sheria itakusaka na jela watakutupa Na utachacha hautotoka miaka mpaka unakufa Sasa chagua nikusaidie kubadilika ama ubakie Na yote ulo'nambia nikusamee sitoyafikiria Unajua pia ni hatia tu kudhamiria kuua Ila I won't press charges nitakuacha tu umeamua Najua hukushiba kwa ndonga walizokupa mtaani Oya mkali na hata hujui unaishi namna gani Haukimbizi shida kisa fake post kwa IG Kinachofanya sisters wanamegwa kabla ID It's all a dream kuna muda sikutaka kuamka Ndoto tamu hadi nikasahau kurauka Amka kijana kuna shuka,yakutupa Shtuka ukiamka ukilala muhindi atakufungulia duka Pia mimi kuna muda nilikua hooker ka wangware Nilikua nakosa dish haki ya mungu hata kahawa ngware Boss hushika nare nikikosa leta ka kitu And I lived with my young sissy ye hutoka wera usiku Ila naamini Opportunity comes in your working clothes Na Subira huvuta kheri that's a simple joke Tujifunze kujitegemea no pillar Hata bila bob,unaweza tu baki kama wailers Alafu Juu ya bundles na vocha, msosi unakosa Kisa kuparty,unarudi ghetto unakopa Mwenyewe unamkosa mwisho unapata broka Unaogopa,amekuwa player unapata coacher You sound cool halafu yanki bado una future mbele Jiulize tungekua na taifa angekata Tamaa nyerere Keep your hopes in the cloud boy unaweza kua cowboy John were,be aware hufanani kua tough boy Hupati kitu leo (hupati kitu leo) Yeah! Just change bro You have a better future I believe in you Start believin' Amani (wala siachii jala leo) Umekosa bro Siachii jala No
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out