Lyrics

Mwamba wenye imara, kwako nitajificha Maji hayo na damu, yaliyotoka humo Hunisafi na dhambi, hunifanya Mshindi. Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria Nijapofanya bidii, nikilia na kudhii Hayaishi makosa, ni we wa kuokoa Sina cha mkononi, naja msalabani Nili tupu nivike, ni mnyonge nishike Nili mchafu naja, Nioshe mi sijafa. Nikungojapo chini, nakwenda kaburini Nipaapo mbinguni, nakukuona enzini Roho yangu na iwe, rahani mwako wewe
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out