Lyrics

Siku moja nilipigiwa simu Ilikua simu ya mwaliko Jumapili tutamshukuru Mungu kwa Sadaka ya pekee Uje uimbe kanisani kwetu Mda ulipofika wimbo ukaimbwa Nao wakaja mbele Wametanguliza kijana na binti mmoja Msemaji wao akaanza kutoa hotuba fupi Kabla sadaka haijatolewa Mungu ninakushukuru sana Kwa. kwa kumponya binti yangu alieugua kichaa Pia ninakushukuru kwasababu kijana huyu alionesha upendo wa ajabu Nilipomwambia achana na mwanangu hakufai tena Yeye alijibu nimempenda ntaoa ivo ivo Sijawahi ona upendo kama huu Sijawahi ona upendo kama huu Upendo. Upendo haupo katika maneno Unaonekana kwa matendo Hauonekani kwenye raha Wathibitika wakati wa shida Daima upendo una sura mbili Japo wengi wanaijua moja Wakati wa raha, faraja na nyimbo na zawadi kede kede wanaridhika na upendo huo Ila upendo una kipimo chake wakati wa shida na raha na wakati wa magonjwa Wakati ambapo waona tabia kasoro na mapungufu hapo ndipo upendo upimwa Yule anaeweza kusimama na wewe wakati wengine kawaida wangekukimbia Tena awezae kukufichia aibu wakati wengine ni kawaida wangekutangaza Yule ambae hapendi kuona unaharibikiwa Hata mkikosana hapendi kuona unateseka Huyo ndie mwenye upendo wa kweli Huyo ndie mwenye upendo wa kweli Upendo upendo Upendo Haupo katika maneno, unaonekana kwa matendo Hauonekani kwenye raha huthibitika. wathibitika wakati washida, wathibitika. Wathibitika wakati wa shida Watu Duniani wanaangaika Kupenda vinavyopendeza Wanasahau kupenda vinavyopendeza hakuna thamani, isipokua kupenda visivyo pendeka Kama mkiwapenda wale wawapendao Mwafanya ziada gani wapendeni waombeeni wanaowaudhi Baba yenu wa mbinguni atawapa thawabu na watu watasema huu ndio upendo wakweli Jipime kama kweli wewe unaoupendo Ulifanyaje Nduguyako alipokukosea Ulimsengenya au ulimuombea Ulimpenda bure au ulimpaka matope Ulimsengenya au ulimuombea Ulimpenda bure au ulimpaka matope Jijibu kama una upendo wa kweli Jijibu kama una upendo wa kweli Upendooo. Upendo haupo katika maneno unaonekana kwa matendo Hauonekani kwenye raha Huthibitika wakati wa shida Wathibitika wakati wa shida Upendo haupo katika maneno Unaonekana kwa matendo Hauonekani kwenye raha Wathibitika wakati wa shida Wathibitika wakati wa shida Kanisa lote lilinyamaza Binti akapewa nafasi aseme Akalia sana... Akishangaa Sijawahi ona upendo kama huu Sijawahi ona upendo kama huu Akalia sana mbele za Mungu, akanyoosha mkono atoe sadaka Najua uliniponya sikwaajili yangu Ukutaka aaibike na upendo wake Ukutaka aaibike na upendo wake
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out