Lyrics

(Uvivu ni adui mkubwa, wa ujenzi wa taifa Kwani ndicho kiini hasa, kisababishacho njaa Ewe ndugu yangu wee, Amka kumekucha, kamata jembe na panga twende shamba Ata wewe mwanangu, amka kumekucha, kwani hizi ndizo za kwenda shule Hata wewe karani, amka kumekucha, Kwani hizi ndizo saa za kwenda kazi) *Bridge* Uvivu, ndiyo adui ya ujenzi wa taifa. Jiepushe, na uvivu tujenge taifa. Ndugu yangu, kumekucha amka wende shamba. Jiepushe, na uvivu tujenge taifa. Mwanangu, kumekucha amka wende shule. Elimu, ndiyo msingi wa maendeleo. Karani, kumekucha amka wende kazi. Jiepushe, na uvivu tujenge taifa. Uvivu, ndiyo adui wa maendeleo. Jiepushe, na uvivu tujenge taifa.
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out