Lyrics

Instrunmental Iye iyee (oooh) iye iye iye iyeee Iye iyee, iye iye iye iyeee Tongwe records baby Wameweka mpira kwapani tayari nishawanawa Ka napiga halafu nafinya namficha shinji kagawa Suka weka kushoto maninja wakachimbe dawa Nina ngunga kama ukoo usipimie hizo sha Aluta kontinua Viva ngoma viva Bwanamdogo anajiita over Mamdogo anajiita diva Ni freemason fever This ridiculos Wauza Papa nguva dili nao perpendicular We si una mengi (it's okey) me ntakusaga Show zangu baunsa anacheza Mchecheto ulimpata jaguar We nianzishe kwenye show nisepe na kijiji Promoter utapigwa mawe na wanaojiita magwiji Mzee kasema hakupi namba na hutaki jiunga vinega Dogo utasugua benchi hutaki sugua gaga Mc hufuati misingi unarukia kama panzi Usifakamie ukadhani maziwa zingine zanzi Sio vita ni changamoto Karibu kikwetu kwetu Chagua ukipenda fursa Ikamate twenzetu Wanatugawa kimakundi watumeze Ona anakonda family lahi wallah Leo jide anamjua songa Middleman mkishndwana cv anaitia gundu Atakula nini mwanangu Lini nitajenga bunju Mkinizima nisikike nitaenda cheza kabumbu Na Roma atabaki juu ata ukiminya mapu ooh Karibu kwenye kalamu We baba uliyepinda mgongo Kiwete mwenye magongo Tupa magongo unifuate Karibuni kwenye kalamu Mama uliyelala juu ya kitanda Unawaza kwenda kwa mganga Imani yako itakuponya Karibuni kwenye kalamu Umejikwaa na umeanguka Nishike mkono inuka Jikung'ute kisha njoo Karibuni kwenye kalamu ooh Karibuni kwenye kalamu Njaa ya madee haifanani na njaa ya ommy wa tupogo Na show akikataa Izzo B atakwenda Ney wa Mitego Huyu anaikataa laki Yule anaifuata kwa basi Yule watamfanyia fitna ang'ae kama almasi Pamoja utatoka wapi kati ya mchicha na mbuyu Wadau wana chenga nyingi kama walichezea Tukuyu Na kufumba macho siyo njia ya kuikwepa ngumi ya uso Nilipotoka ni mbali enzi nadandia mafuso Unaweza sali uzae chema ukazaa shoga na msagaji Mpagani akabakwa ikatunga mimba akamzaa padri Hili Mungu atukuzwe wote hawakuja kumzika sharo Hamuoni Yesu alilia alipokufa lazaro Na kabla Yesu hajarudi angerudi Nyerere mzee Ashuhudie madhabau yakigeuzwa uwanja wa harambee Hawakemee baba askofu wachungaji mashekhe Wanaogeuza injili mtaji washindwe na walegee Ukisema ukweli wanakuzika kama analog kwenda digital Nashukuru nahema Mungu niepushe na tindikali Nafunga na kusali litania ya bikira Maria Piteni mbali nimetumwa na parokia Tusipigane mapanga kubishana nani achinje Wananidiss na bado unialika kwenye kilinge Usiponipiga me nitapigwa hata na bajaj za mwenge Nina msimamo kama kama tongwe yeah yeah Karibuni kwenye kalamu Dada uliyemaliza chuo Umepass na huna kazi Vibebe vyeti nifuate Karibuni kwenye kalamu Nyuma ya nondo ya gereza Sauti yangu iwafariji Ipo siku mtatoka kisha Karibuni kwenye kalamu Ona wazazi wamekufa We ndio baba we ndio mama Familia inakutazama Karibuni kwenye kalamu yeah Karibuni kwenye kalamu Ona me mzalendo mwenye mapendo Nakemea wenye biashara ya magendo Wanasema wamepinda kama mizengo Wanasinzia kwenye mijengo Ona me mzalendo mwenye mapendo Nakemea wenye biashara ya magendo Wanasema wamepinda kama mizengo Wanasinzia kwenye mijengo Kambarage hakuwa chadema lakini alivaa kaki Kuna wabunge uwa najiuliza wanavuta bangi ya wapi Bongo movie ni bunge movie Tuitazame tamthilia Viongozi wanashuka hadhi kwa kugeuka mabondia Kukosa amani sio mpaka ugombane na nchi jirani Polisi akimuua raia ni vita vya ndani kwa ndani Rasilimali isiwe mali ya serikali Mwekezaji epuka mgogoro wa ardhi Mkulima na mfugaji aliyepata zero form four Mnamsukuma aende veta Mnaamini umeme wa magari ndio unahitaji mazezeta Yashinde majaribu jela uliyefungwa kwa hira Sali milango ifunguke design ya Paulo na sila Anakula kwa mipira anahema kwa mashine Nani alitunza bikira hadi siku anampata mume Kama uliupasua mpira usiuze mechi karatu Kuwa mvumilivu wa subira kama mama anayecheza upatu Binti ametega mimba na wewe unajiona shababi Kakuona ganda la ndizi Na kwako beki hazikabi Kuwadi anamfunda mwali Sina amani na huyu kungwi Hiyo pesa ya mchango wa harusi bora nisagie mirungi Kadi hawapewei so usiogope hayo magari wanahongwa Shosti ukaibeba sembe kizembe china utanyongwa Maisha foleni umangaribi uache ukaipande tonda Ukiwaiga walioiua meli ipo siku utaiua nyonga Siogopi mainstream na post ya kuvuka boda Wanangu wa boda boda pigeni nyie ndio ma soldier I told ya Maadui wapo kimbiji Na me nimeaga Tanga navuka boda ya Msumbiji Tongweoooh Ona me mzalendo mwenye mapendo Nakemea wenye biashara ya magendo Wanasema wamepinda kama mizengo Wanasinzia kwenye mijengo Ona me mzalendo mwenye mapendo Nakemea wenye biashara ya magendo Wanasema wamepinda kama mizengo Wanasinzia kwenye mijengo ...Tongwe records baby
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out