Lyrics

Niamini (Sema) Nataka uwe na mimi (Mama) Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye) Hivi kwanini (Sema) Hutaki kuniamini (Mama) Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye) Niamini (Sema) Nataka uwe na mimi (Mama) Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye) Hivi kwanini (Sema) Hutaki kuniamini (Mama) Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye) Nakupenda sana ingiwa wanakuita demu wa uswazini Penzi lako la kweli ndo kitu nachothamini Kipepeo cha moyo we sema unachotaka Jinsi unavyoenzi kipenzi sina mashaka Tulipanda milima tukaja kwenye mabonde Na sasa ni tambarare tufanye wanga wakonde Kote tunakopita wamemwagia mbigiri Njoo nikumbatie tufe tukiwa wawili Hushangai, tukigombana tu wanafurahi Na tukiwa pamoja wanashindwa kutusabahi Walishakuja kwangu kunipa habari zako Nikawatoa mbio kulinda heshima yako Kwangu wamenishindwa wamegeuza kibao Changanua mapema upime akili zao Ni maisha yo Liz, twende tujikongoje Maisha safari ndefu sijui mbele kukoje Wanasema mi nakunywa wee, nalala kwenye baa Wanasema mi ni bingwa la ngono kwenye mitaa Wanasema mi nimeshawataka wamekataa Kwako napiga goti yoh twende ki-superstar Niamini (Sema) Nataka uwe na mimi (Mama) Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye) Hivi kwanini (Sema) Hutaki kuniamini (Mama) Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye) Niamini (Sema) Nataka uwe na mimi (Mama) Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye) Hivi kwanini (Sema) Hutaki kuniamini (Mama) Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye) Yoh, nikwamba Mi nashukuru sana, umeniamini kwa sana Hukufata maneno ya wanga waliochonga kwa sana Miss Manana baab kubwa, hiyo ndo dhana Wala hukunikana asante sana mi sitokukana Tulifarakana tulikaa chini, tukapatana Bila kugombana na ndio maana hatujatengana Tukasamehana bila kutosana, endelea kukazana Visa vizabina maji ya shingo sa chupi zinabana Vichwa vinagongana wanaulizana, hatujaachana Wanapigwa na bumbuwazi kuona bado tunakumbatiana Tunashirikiana, na tunafanya vitu vya maana Na haki ya Mungu nakuahidi mi ndo wa dhamana Nakata mzizi wa fitina we ni wangu wa kuzikana Mwingine hakuna, vita vya manyoya sasa hapana Kwani maneno yalizidi hasa kwa wanga na mahasidi Na wengine waliahidi lazma watumwagie acid Eti hakomi kutupwa na napiga sana mchupa Hautachukua round kwangu mi ntakutupa Haukufanya pupa haukuogopa, hungenichoza Ya Mungu mengi leo hii kwetu mambo ni super Na yote aliyoahidi kwako mimi lazima nitakupa Usiwe na pupa, tulia, mi ndo simba Unanipaga hamu, na hilo napenda ufahamu Nakumbuka maneno yako matamu, mi nakupenda wewe Unanipa kiwewe, ubavu wangu wa pili ni wewe Napenda uelewe, niamini ni mimi na wewe Niamini (Sema) Nataka uwe na mimi (Mama) Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye) Hivi kwanini (Sema) Hutaki kuniamini (Mama) Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye) Niamini (Sema) Nataka uwe na mimi (Mama) Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye) Hivi kwanini (Sema) Hutaki kuniamini (Mama) Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye) Amini amini, tuko pamoja safarini Wala sigeuki, nipo makini na wenye chuki Hivi ujabaini? Wanakudanganya maneno lukuki Eti napenda chini, eti nakuhasi na hugutuki Hivi inaingia akilini, Ni muda gani na ni lini? Siku hiyo hatukuwa pamoja? Kama si huzushi ni nini? Wanga wanajikongoja navyokupenda kwa ukalando Mwana wametunga hoja, tutengane iwe furaha Iwe tazamia vioja, usiwaamini mara moja Wengi ni vizabi zabina, wapiga majungu na wafitina Magwiji washirikina, pima vyema tena kwa kina Tusije tukaachana, tutawapa msemo wageni iwe meno Itakuwa haina maana, mara tu tumefarakana Pia itakuwa aibu, tujaribu kuvumiliana Mapenzi ni taratibu, mambo ya jana sio ya leo Tusije tukaharibu, hebu sikia sogea karibu Nani wa kunigiribu? Kwako sioni, sisikii Ukiacha utaniadhibu, we nipe raha, nipe dhabibu Mpaka ntakapokufa, tushirikiane kuziba ufa Wanga wasitufate, nafurahi unavyonipenda Usije ukasema asante, we nipe denda, nipe mate Mama subiri fungate, mzizi wa fitina tena tukate Wewe na mimi (Mimi), niko radhi kula yamini Wewe na mimi (mimi), mama Lily hebu niamini
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out