Lyrics

Prof Jay: Nawashukuru sana wananchi kwa Kweza kunipa kura Nashangaa nimeitwa ghafla kwenye Kikao cha dharula Kikao kinaashiria kina maswali juu Yangu Hii inatokana na ndiyo mzee na ahadi Zangu. Naona watu ni wengi wananchi walio Na maana Najaribu kutafakari ni nini Kinawachanganya!! Nipo tayari kujibu maswali yenu zamu Kwa zamu Watakao uliza maswali na ningependa Niwafahamu .Naitwa sajent Byemero kwa niaba ya Jeshi la polisi Nilikuwa nauliza zile helikopta zetu Vipi? Prof Jay: Nafikiria kwanza kuanzisha chuo cha Marubani Vinginevyo mtapata ajali nyingi sana Angani. Baskeli hamjui kuendesha helikopta Mtaendeshaje Kila mtu aendeshe yake huko angani Itakuwaje? Mheshimiwa sisi wakulima ulituahidi Matrekta Na siku zinayoyoma tu mbona Haujayaleta? Prof Jay: Wakulima mngeendelea tu kutumia Jembe la mkono Serikali haina hela bajeti imefika Kikomo Naona kilimo cha mkono kiniendelea Vizuri Jamani kazeni mikono endeleeni Kukaza misuli KIITIKIO Wananchi tupo pamoja hapo. (siyo Mzeeeeeee) Watanzania tunaerewana kule, (siyo Mzeeeeeee) Washika dau na wapiga kura pale (siyo Mzeeeeeee) Eeehh: siyo mzee... eti, (siyo Mzeeeeeee) Wakulima tupo pamoja pale, (siyo Mzeeeeeee) Wanafunzi tunaelewana kule, (siyo Mzeeeeeee) Mabahamedi na mapolisi pale (siyo Mzeeeeeee) Prof Jay: Mabaaamedi ondoeni hofu kilio chenu Nimekisikia Ma benzi yenu yapo bandarini tayari Yameshawadia Nimemchagua kiranja ili anipe idadi Yenu Niwape funguo zenu muondoke na Magari yenu. Ulituahidi utatujengea barabara tano Tano juu na chini Hizo zote hatutaki tunataka moja tu Ardhini Kila siku tunapita barabara zinakuwa Mbaya Umeyafumbia macho mheshimiwa Huoni haya? Prof Jay: Barabara ya makwekwe nimesha Imwaga kifusi Baada ya wiki mbili itakuwa safi kama Urusi Makandarasi wanafanya kazi kutoka China na madagascar Kuhusu vibarabara naomba muondoe Shaka. Eeh vipi mzee mabomba kutoa maji na Maziwa nchi nzima? Prof Jay: Jamani naomba muulize maswali ya Utu uzima Mabomba kutoa maji na maziwa Haiwezekani Mlinukuu vibaya nasisitiza haiwezekani Mzee hali ni mbaya si tungegawana Vya kwako? Kwenye kampeni zako si ilikuwa moja Ya ahadi zako? Prof Jay: Eeehh? kugawana vya kwangu hilo Swala litakuwa gumu Familia itanitazama ebo? nina Majukumu Imeandikwa kila mtu atabeba msalaba Wake Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba Yake Mbona mnaniuliza maswali mengi Kunikomoa Jamani watanzania tunajenga Tunabomoa RUDIA KIITIKIO x2 3 Prof Jay: Wafanyakazi wa serikalini sasa nyinyi Magari ya nini? Daladala chungu mzima mnaweza Kuwahi kazini Nasema mnapenda sana starehe kuliko Kazi Na hiyo ndio sababu mnaharibu hiki Kizazi. Wanafunzi niliwahidi mtafanyia Practical mwezini Kabla ya kupeleka mi nilifanya utafiti Nimengundua huko mwezini kweli kuna Baridi sana Na pia kunavitisho kuwepo kambi za Osama Mkinichngua tena mtakwenda huko Mapema Nanita tekeleza kila neno ninalo sema Sema nimesongwa na haka kamuda Mkiniongezea muda kila kitu babu Kubwa Wengine kimya na maswali Yamepungua Yeyote mwenye swali ningependa Kumtambua. Naona mnanong'ona na wengi Mmekunja sura Hii inaonyesha mmeridhika kunipa kura Nadhani ndugu zangu tuko pamoja... (Aagh wapi) Jamani tupunguzeni jazba basi Kidogo... (hatutaki) Sasa watanzania mbona mnaazisha Vurugu Nadhani mmesahau watanzania wote Ni ndugu Babu Ayoub: Eeeh? jamani nasema hivi kikao Kimeahirishwa Jamani maafande... Afande miraj... Afande mzafalu, Afande nani Gondwe njooni mtusaidie Huku. RUDIA KIITIKIO X2
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out