Lyrics

Nakuambia, aah siri yangu Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi Nakueleza, aah siri yangu Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu Tega sikio kwa makini nikueleze Hakuna tamu penzi kama la milele Muda unaenda mwenzenu mi nagundua Moyoni mwangu katu halitopungua Nimeumizwa mara nyingi nakumbuka Kuna hatua ilifika mi nikajuta Lakini sasa 'na imani yupo wa kumpa Ninachohitaji ni muda aweze tokea Siwezi sema kuwa sitopenda tena Kwani nitakuwa naidhulumu yangu nafsi Moyoni najua ninalo penzi la milele Na halitokwisha nakwambia labda wa kumpa asizaliwe Nakuambia, aah siri yangu Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi Nakueleza, aah siri yangu Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu Kuna aliyeniomba nimpatie pumziko Kwa madai kuwa alichoshwa huko atokako Niliyempenda nilimwambia nakupenda Nililia machozi kwa yeyote aliyenitenda Aliyenichosha nilimwambia waweza kwenda Kuna aliyenifanya mapenzi yakanitatiza Niliyemkosea niliona umuhimu wake Nasisitiza kuwa 'na penzi la milele Moyo wanituma wan'ambia kuwa na subira Mimi nasema sitoimba tena nalia Iliyobaki ni kusema nimekubali Sitokaa tena kulia mimi na mawazo Nakuambia, aah siri yangu Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi Nakueleza, aah siri yangu Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu Unaweza toa pendo lako kwa furaha Kumbe moyoni umejijazia karaha Hutakiwi juta kwani katu hutojua Unayempenda yeye atakuzingua Mwisho wa yote ikawa ni matatizo Yanayopelekea kuwa na mengi mawazo Unachotakiwa, binti, usiusemee moyo Kwani hutojua umpendaye naye akupenda hivyo hivyo Niliwahi kumwimbia mpenzi wangu "Sema unachotaka" ni wimbo uliofuatia Lakini pendo hakuna bali ni kutendwa Nimeamua kuwa komando Binti Machozi Nakuambia, aah siri yangu Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi Nakueleza, aah siri yangu Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out