Lyrics

Siwema usinipe mateso ya moyo Na sasa nimechoka kweli nasema Siwema usinipe mateso ya moyo Na sasa nimechoka kweli nasema Nilidhani nimepata mpenzi wa kweli Nakumbe nimepatikana na mambo ya ajabu Nia na madhumuni yako nimeshavitambua Siwema kaka Siwema kaka, ah ah ah Unajitapa mbele ya rafiki zako Kwamba mimi sina la kusema mbele yako Umeniweka kwenye kiganja mama Unalotaka ndilo ninalofanya Sababu wewe ni mzuri sana Siwezi kupata mwingine kama wewe Siwema kaka, unajidang'anya Wema wangu ndio ulioniponza Fadhila zote, kumbe kwako ni bure Malipo yake, kunifanya mjinga oh ooh Hayo yote ni makosa yangu Lakini sasa nimejifunza kutokana na makosa Najiepusha nawe mama aah Nimezunguka Tanzania bara Unguja na Pemba nimefika aah Nimewaona vijana wenye sifa aah Wenye kujipamba wakapambika, aah Nimezunguka Tanzania bara aah Unguja na Pemba nimefika aah Nimewaona vijana wenye sifa aah Wenye kujipamba wakapambika, aah Kwahiyo nielewe brother (Sibabaishwi na sura napenda tabia njema) Sibabaishwi na sura yako (Sibabaishwi na sura napenda tabia njema) Usifikiri mimi rimbukeni sana (Aah, sura napenda tabia njema) Nilikupenda kimapenzi (Sibabaishwi na sura napenda tabia njema) Ukaniona mimi sugamami lako (Sibabaishwi na sura napenda tabia njema) Tabia njema ndio silaha yako (Sibabaishwi na sura napenda tabia njema) Kila mtu atakupenda kaka (Sibabaishwi na sura napenda tabia njema)
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out