Lyrics

It's Rostam baby Tongwe records baby (Bin laden) Nakusalimia kwa jina la jamhuri ya Tanzania Siku nyingi hatujaongea na sisi ni familia Na mbona hukuja kumzika baba, kwa nini? Ukipata muda kasome Luka 9 mstari wa 60 We nae umezidi utukutu ndio maana baba alikuchukia Wengi tulioko huku mioyo yetu iliumia Kuona baba akiwakemea waliotuonea aliwasifia Mwenzangu ulipendwa sana, nyimbo zako alifurahia Kaka marehemu hasemwi njoo tujenge familia Acha niondoke nina damu ya kunguni nisije nikajifia Tunaimba wote nafungiwa mimi? Umesahau ya kibamia? Ila sasa unaweza ukarudi (Mmh) Hata kaka aliyekuwa hakupendi Mambo yake yako mshazali (Wacha) Aliuza nyumba ya kino bila hela ya udalali Akapata ya Kigamboni kasombwa na upepo wa bahari Hii ni hatari kuna watu baba aliwapa kiburi Tulionekana wajeuri kila tulipo mshauri No na wasiwasi na walio baki mama awaangalie vizuri Kama? Kaka yetu aliye hai na yuko happy? Yule chenga Polepole haya mambo sasa ni msiba Njoo chemba (Narudi Januari na nitafika kwa kaka Bumbuli) Hata kwa mamdogo yule mwalimu wa tanga utaishi vizuri Mama tuna kutazama we Mama tufute machozi Mama mama mama Kila mtu anasema lake hivi kipi kime muua baba? Achana na maneno ya watu na tena badirisha mada Ni maradhi ya moyo usisikilize hizo kelele Muache baba apumzike kwenye nyumba ya milele Tafadhali msisitize asiache kuvaa barakoa Mama yako yupo majukumu ndio yamembana Na juzi kwenye kikoba wamempa uwenyekiti wa chama Na nimewapenda sana wale wasaidizi alio wachagua Waliopita ni wezi wa vikoba yani afadhali amewatimua Na kikoba cha vijana bado anakiongoza kaka Mmh yule sidhani kama mama atamuacha nina mashaka Hivi vipi huko umeshaonana na dada? Maana hata yeye ilikuwa haziivi na baba Dada amechoka wanafamilia wana mwangusha Ila nitaonana nae sisi ni ndugu siwezi kumsusa Shauri zenu bwana tukipewa urithi msishangae Emhee yani toka nikujue leo ndio umeongea cha maana Nina mengi ya kukuuliza smije mkamdhulumu mama Vipi swimming pool ya babu ile ya Rufiji? Sasa hivi iko chini ya nani na inamnufaisha bibi? Baba alisimamia katuachia sisi wanae Na kumewekwa mataa yanayo imulika Kisarawe Na ile biashara ya Bagamoyo baba alioisitisha? Juzi mjomba alisema iendelee inasikitisha Mama amuwangalie kaka yake kwa makini atamfelisha Mama tuna kutazama we Mama tufute machozi Mama mama mama Rudisha tabasamu Baba alifanya mema mengi muacheni alale Oya saa ngapi huko? Unasikiliza ngoma za kale? Natamani kuisikiliza ya kwelina kwenye daraja la Mfugale Njiwa wametutia hasara sijui aliwaza nini baba? Kivipi? Wakati naondoka mi niliwaacha wako saba (Mama akaongeza watatu) njiwa mkubwa hatagi kwa nini? Lile banda kule kijijini sa baba alilijengea nini? (Mwe makini na yule baba mdogo mchungaji) Mama yupo sehemu salama usijali punguza uwoga Na ushauri pia anapewa na baba mkubwa wa Msoga Halafu baba na yule Uncle wa Singida hawakupatana Kwa nini wasikae wamalize tu tofauti zao na mama Ndio uongee nae sasa harudi si unajua kuwa alihama Yeye na rafiki zake wapate usalama Na wale nashangazi wawili bado wana hasira na baba Wangesamehe na kusahau wangempa mama msaada Na umwambie mama aendelee kushirikiana na majirani Familia ina amani waliokwazwa warudi nyumbani Naona kikao cha familia kina ndugu wa upande mmoja Uncle anawajibu ndugu wa nje na kuacha kujadili hoja Ebu kwanza ngoja mama anaingia tutaongea baadaye Nitakucheki ngoja nimpe simu uongee nae "Halloo hujambo mwanangu..."
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out