Listen to 2030 by Roma

2030

Roma

African

6,544 Shazams

Lyrics

Instrunmental Tanzania eeeeh (tongwe records) Nchi yangu oooh Huwezi kuijenga Roma, haikujengwa kwa siku moja Iwe kwa raha leo au simba mtoto Tanga watakuja Hata Patcho pia ni mwamba ila bado anakata viuno Kaskazini bila Tanga ni msondo bila Gurumo Alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa na halitatikisika Waumini tuianze misa Kwenye njaa kula kuku aliechinjwa na padri awallah Adhana ikilia amka ukamwombe Allah Bwashee mrudie Mungu Masanja kawa mchungaji Sujudu Makka madina tajiri hataki kuhiji Maulidi Ubungo kibangu ndo mishahara ya madrasa Ona rafiki wa padri kawa muhasibu wa kanisa Tenda wanapeana kindugu mwanangu kua uyaone Familia ilikata ringi na mama alibaki mjane Sikuwa na damu ya kiarabu kwamba ntarithi mabasi Dingi hakutupa msingi ona gari twaifanya taxi Tazama Gongo la mboto mtoto kamzaa mtoto Na atalelewa na nani baba ake mmemfunga keko Wape buku waue winga wale watoto wa Morocco Mungu atazidi kulinda kesho utaiona sabato Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani Ana wake wake watatu je watoto watarithi nini Ndo chanzo vha kurogana na kutupiana majini Huyu akimpandisha makata hule maimuna subiah Maana pesa ndo ilifanya tusiwe na Tanga ndugu Pesa ilileta ubaguzi kati ya Loyola na Pugu Pesa ndo ilichochea bifu ya Nice na Dudu Na pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu Tanzania eeeh Mwanangu kua uyaone kama ntawahi kuiona paradiso mtunze mama ako Nchi yangu oooh Mwanangu kua uyaone marehemu hufa na chake pigana upate chako Tanzania eeeeh Mwanangu kua uyaone mwalimu cheza kibati wanao wasife njaa Nchi yangu oooh Mwanangu kua uyaone elimu imekosa thamani necta imevuja kibaha Aminini nawaambieni ujana ni maji ya moto Mtoto humzika mama leo mama anamzika mtoto Ndo maana mama alisema nisimchumbie Mmachame muraa shusha mapanga naileta posa Tarime Leo bahari imechafuka mpemba iheshimu karafuu Hatari kama Nungwi nahodha sio kirikou Yahee nirushie mtumbwi Me mwamba sio kichuguu Hii ni vita ya msambaa mbodei usitie maguu Ona kipindi cha bunge Dodoma inanuka ngono Spika akiahirisha bunge wengi watausapoti mgomo Wabunge mnadai posho, muhonge dada zetu Kuna wanafunzi wa mama salma vyuoni usicheze peku Wazanzibar hawaioni thamani ya huu muungano Ila kulichoma kanisa sio njia ya kuvunja agano Sioni sababu ya ubaguzi na kuua wasio na hatia Wakati aliochanganya mchanga, mchanga umeshamfukia Muislamu gani unahonga bongo movie mamilioni Mama anakufa mwaisela kakosa drip ya quinine Ni kheri ujenge msikiti tuitukuze mitume Anasa za bakurutu unawatuza wacheza sebene Unamuheshimu ramadhan unazini mbele ya shaban Kama ilishushwa kuran twendeni misikitini Anaedhihaki msaafu pengine kanisa halijui So kulichoma kanisa ni kuuza bible Dubai Usihofu kumpoteza mmoja ili kumi waishi vyema Watanzania tuna uoga sio amani mnadanganywa Sacrifice for your son and daughter amka kifikra Damu yako iwe chachu ya ukombozi Dr Ulimboka Mjinga usimuue mama ili uongeze kipato Utajiri upo kaburini watu wamekufa na ndoto Leo Ridhiwani hafanani na Makongoro Dah sina hela ya kiroba Rashid nigongee ugoro Suka kaiangusha lorry ya mafuta yote magendo Waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya tembo Nchi imejaa misitu tuna uhaba wa madawati Tunakula vitu feki (what) TBS mko wapi RPC usitume kikosi ili uishushe chadema Italipwa damu ya Mwangosi Iringa semeni amina Okoa wagonjwa wa saratani mpakani zuia wakimbizi Kuliko kumwaga pesa kwenye tume za uchunguzi Muhimbili naumwa goti eti dokta kapasua kichwa Mbeya wanapigwa nyundo ili raia wauze mabucha Amana wanatelekeza watoto wanalia Mwananyamala wanatuua na hawaendi jela jela anaenda Kajala Tanzania eeeeh Mwanangu kua uyaone cashier acha kisirani ngonga muhuri tuwahi Nchi yangu oooh Mwanangu kua uyaone mnafki hasira za mkeo barabarani hazifai Tanzania eeeeh Mwanangu kua uyaone wanahonga mashabiki ngoma zao wazi repaste Nchi yangu oooh Mwanangu kua uyaone udini wa mapresenter wapagani unatukosti Sauti hii itasikika mpaka Oldonyo lengai Nikifa naomba nizikwe Tanga na mje kwa shambalai You can tell me bro but won't kill what I'm standing for Siutamani urithi wa baba ikimshuka CD 4 Eti tuzo sikustahili hahaaa hii ni hatari Tuzo ina chapa ya nani ya kaisari mpe kaisari Me sio masaki ni ngaramtoni mama anaiuza dadii Muziki umejaa stress kila nyuma ina msanii (oyoooo) Yanga wamemfukia mbuzi golini Simba wana bundi Viongozi wanataka umate umate hawaujali ushindi Utaskia Chuji kachuja jamhuri choma mahindi Kapigwa ligi ya jogoo shahidi kamati ya ufundi Vijijini tuko wengi mleteni daktari bingwa Ana ngoma uyasikia karogwa twende kwa mganga Pesa za kujikimu nd ulichongesha kitanda Kulea mimba sio mchezo baba kijacho haujajipanga Profesa kanyimwa penzi utaskia Calo kadisco Na Caro analea ndg kwe pesa ya bodi ya mikopo Pole mnaotafuta C mwaka wa nne mnarisiti Huku headmaster kaenda mjini eti shule imeiahiwa chaki Msiwaue wachimbaji wadogo Geita inalia Kaburu umempa migodi UDSM tuna engineer Unapewa kontena la kondom uihonge dhahabu MV spice ilipozama TV inaonesha taarabu Kamanga hawaiweki lami ili tuvukie Busisi Dereva usinitoe kafara ili utimize hesabu ya bosi Sina cha kuweka rehani kwenye asasi za mikopo Bajeti ya kilimo kwanza mkulima silioni soko Tanga mmekosa nini amkeni acheni umwinyi Hawa wachaga hawatuwezi ona Manka balaishirini Bandari chanu railway chali Makamba iinue katani Zitto akirogea Kasuru si tunamrogea Pangani Uchafu wa Mrisho unafanya msafi aonekane Benja Sisadiki magazeti waandishi wengi kanjanja Vijana ndo nguvukazi ila wengi wamejali utindi Mtaani wamekata ringi haki msingi wanaziweka bond Majibu ya postmortem kashanunua wakili na Hakimu kapewa kiwanja kimara apige kufuri Cheki dola wanainunua kesi napewa kapuku Nna upole kama ngamia mbele ya hakimu wa kisutu Tanzania eeeeh Mwanangu kua uyaone Nchi yangu oooh
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out